Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:45

Kizingiti kikuu katika mazungumzo ya Kongo ni wadhifa wa Waziri Mkuu


Askofu Marcel Utembi, kushoto, Rais wa Baraza la kitaifa la Maskofu Kongo akiwa pamoja na Askofu Fridolin Ambongo mjini Kinshasa, DRC, Disemba 21 2016.
Askofu Marcel Utembi, kushoto, Rais wa Baraza la kitaifa la Maskofu Kongo akiwa pamoja na Askofu Fridolin Ambongo mjini Kinshasa, DRC, Disemba 21 2016.

Ujumbe wa upatanishi wa mazungumzo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya serikali na upinzani, umeleza Alhamisi kwamba, kizingiti kikubwa kuweza kufikiwa makubaliano ni wadhifa wa waziri mkuu, kuachiliwa kwa wafungwa wa kisasa na kuruhusiwa kurudi nyumbani wanasiasa walio uhamishoni.

Ujumbe huo wa Maaskofu wa Kanisa la Katholiki, ulikutana na Rais Joseph Kabila Ikulu siku ya Alhamisi Jioni baada ya kukutana na Spika wa bunge la taifa Aubin Minaku.

Ujumbe huo ulipanga kukutana tena na kiongozi wa muungano wa upinzani Rassamblement Etienne Tshisekedi, katika juhudi za kutanzua mvutano ulobaki kabla ya mkataba wa kuunda serikali ya mpito kutiwa saini Ijumaa alasiri.

Mbunge na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Delphin Kapaya ameiambia Sauti ya Amerika kwamba kuna matumaini makubwa viongozi hao wawili wataelewana na kufikia makubaliano.

James Sawn, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya KIdemokrasia ya kongo
James Sawn, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya KIdemokrasia ya kongo

Katika tukio jingine balozi wa Marekani nchini Kongo James Sawn, amezihimiza pande zote kujaribu kufikia makubaliano kwa haraka ili kuhakikisha mpito wa amani kuelekea uchaguzi mkuu.

Balozi Swan alikutana na spika wa bunge Minaku siku ya Alhamisi ili kuwasilisha ujumbe wa serikali yake kuwataka wadau wote wa kisiasa huko Kongo kufikia makubaliano yatakayohusisha pande zote.

XS
SM
MD
LG