Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:49

Misri imethibitisha kumkamata mwandishi wa kituo cha televisheni cha Al-jazeera.


Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi huko Sharm el-Sheikh, South Sinai, Machi 29, 2015.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi huko Sharm el-Sheikh, South Sinai, Machi 29, 2015.

Misri imethibitisha kwamba imemkamata mzalishaji wa kituo cha televisheni cha Al-jazeera, kituo cha utangazaji ambacho kwa kiasi kinafadhiliwa na familia inayotawala ya Qatar, kwa kwa habari za uchochezi kwa niaba ya taasisi hiyo ya habari.

Wizara ya mambo ya ndani imemtaja mtu huyo kuwa ni Mahmoud Hussain, ambaye alikamatwa Ijumaa kwa shutuma za kuvuruga usalama na kusambaza taarifa za uongo. Al-Jazeera ilisema Misri ilimkamata Hussain kwa mashtaka ya kutunga, baada ya kusafiri nchini humo kwenda kuitembelea familia yake na inataka aachiliwe huru mara moja.

Tukio hili ni la karibuni katika mfululizo wa ukamataji waandishi wa habari wa al-Jazeera nchini Misri, ikiongeza wasi wasi mkubwa juu ya uhuru wa waandishi wa habari wanaofanya kazi nchini humo.

XS
SM
MD
LG