China ilirudisha kwa Marekani chombo kisicho na nahodha inayotumika chini ya bahari ambayo iliikamata wiki iliyopita katika maji ya kimataifa ya eneo la South China Sea.
Msemaji wa Pentagon, Peter Cook amesema makabidhiano ya chomo hicho yalifanyika katika eneo ambalo China iliknyakua ilipokua inafanya uchunguzi katika bahari ya South China kupima kiwango cha chumvi na mabadiliko ya hali ya joto.
“Tukio hili linakinzana na sheria za kimataifa na viwango vya weledi wa namna majeshi ya majini yanavyotakiwa kufanya kazi yao,” alisema Cook katika tamko rasmi.
“Marekani imeshaweka wazi ukweli huu kwa China kupitia mikondo sahihi ya kidiplomasia na ya mawasiliano ya kijeshi, na imeitaka serikali ya China kutenda majukumu yao kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kuepukana na juhudi za kuzuia shughuli halali za Marekani.”
Wizara ya Ulinzi ya China imesema Jumanne kuwa kurejeshwa kwa kifaa hicho kumekwenda vizuri baada ya mazungumzo ya kirafiki baina ya nchi hizo mbili.
Msemaji wa Wizara ya Mambo Nje wa China, Hua Chunying alisema baadae kuwa Marekani imekuwa ikiendesha zoezi la kijeshi karibu na fukwe za maji ya China, jambo ambalo China hawakubaliani nalo.
China imesema harakati hizi zilianza wakati moja ya vyombo vyao vya majini vilipokiona kipande cha kifaa ambacho hakikuweza kutambulika katika maji yao na kukichukua kwa ajili ya kulinda usalama wa usafiri wa majini katika eneo hilo.
Kitendo hicho kiliamsha hisia mpya kwa Washington na kati ya marafiki zake kuhusu China kuweka majeshi yake katika South China Sea, na kile wapinzani wa Beijing walichokiita utumiaji wa nguvu kujibu madai ya harakati za ushindani wa majini katika eneo hilo.
Brunei, Philippines, Vietnam na Malaysia wote wanadai haki ya kutoa madini na kuvua katika eneo hilo, na mengi katika madai yao yanaingiliana.