Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:18

Mabasi ya kuwahamisha wakazi yaingia Aleppo


Wapiganaji waasi na wakazi wakusanyika pamoja wakisubiri kuhamishwa kutoka eneo moja la mashariki ya Aleppo, linaloshikiliwa na waasi. Aleppo, Syria, Dec. 16, 2016.
Wapiganaji waasi na wakazi wakusanyika pamoja wakisubiri kuhamishwa kutoka eneo moja la mashariki ya Aleppo, linaloshikiliwa na waasi. Aleppo, Syria, Dec. 16, 2016.

Shirika la habari la Syria, SANA, linaripoti kwamba mabasi ya kuwahamisha wakazi wa Aleppo yanayosimamiwa na Hilali Nyekundu na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, ICRC, yameingia katika mita ya mji huo uloharibiwa na vita Jumapili asubuhi kuanza kazi ya kuwaondowa wakazi walobaki na waasi.

Wakazi wakipita kwenye vifusi vya mji wao wakibeba mizigo walobaki nayo.
Wakazi wakipita kwenye vifusi vya mji wao wakibeba mizigo walobaki nayo.

Maelfu na maelfu ya wasyria wenye hofu na waasi walokwama huko wamekua wakisubiri zowezi la kuwahamisha kuanza tena. Mapema Jumapili msemaji wa ICRC Elodie Schindler, aliwapa matumaini aliposema,"kamati yetu iko tayari kuanza tena kazi ya kuwaondosha watu kutoka Aleppo mashariki kuanzia asubuhi ya leo".

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura Jumapili mchana juu ya ikiwa iwapeleke wafuatiliaji katika mji huo mkubwa wa Syria uloharibika kabisa kufutilia zowezi la kuhamishwa watu pamoja na kuwasaidia kwa kuwapatia ulinzi raia walobaki.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza litazungumzia pia mswada wa azimioulotaryarishwa na Ufaranasa unaoeleza kuzorota mzozo wa kibinadamu ndani na karibu ya mji huo na haja ya maelfu ya wakazi wa Aleppo wanaohitaji msaada na kuondolewa huko.

XS
SM
MD
LG