Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 20:14

Polisi Tanzania waendelea kumshikilia muasisi wa Jamii Forum


Maxence Melo muasisi wa Jamii Forum
Maxence Melo muasisi wa Jamii Forum

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa jamii forums (JF) Maxence Melo anaendelea kushikiliwa katika kituo cha Polisi cha kati kanda maalumu jijini Dar es Salaam kwa siku ya nne sasa.

Wakili wake Bernedict Ishamakaki amesema hadi Jumatano jioni alikua bado yuko katika mikono ya polisi kwa tuhuma kwamba amezuia uchunguzi wa polisi kwa kuwanyima taarifa muhimu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:13:23 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

“Lakini hakuna kosa linalomnyima dhamana kwani ni makosa yale yale yaliyokuwa yanamkabili siku za nyuma ambayo tulikuwa tumeyaombea ufafanuzi kutoka mahakama kuu,” amesema Ishamakaki.

Amesema kwamba katika barua za awali ambazo jeshi la polisi lilimuandikia kumtaka atoe taarifa zinazohusiana na wanachama wake.

Lakini wakili huyo alieleza kuwa sheria ya mtandao imeeleza habari feki kama ni kosa la jinai, akihoji kwamba ni nani ambaye anaamua kwamba hili ni kweli na hili ni uongo katika taswira hiyo.

Kwa mujibu wa mwanasheria huyo, ziko taarifa ambazo zimetolewa na watoboa siri kuhusu makampuni binafsi ambazo zinazituhumu kampuni hizo kwa ukwepaji kodi na vitendo vya ufisadi.

“Tunasikitishwa kutokana na kuzungushwa kwa mteja wetu na kupigwa dana dana kuhusu dhamana yake, ambapo leo tayari imefikia siku ya tatu,” alisisitiza Ishamakaki..

Alisema kwamba sera za jamii forum ziko wazi tangu ilipoanzishwa mwaka 2008, kama ingekuwa inahatarisha usalama wa taifa ingekuwa imefungwa zamani.

Simon Mkina msemaji wa Jamii Forum
Simon Mkina msemaji wa Jamii Forum

Kwa upande mwengine msemaji wa JF, Simon Mkina amethibitisha kwamba uchunguzi ungali unafanyika kulingana na polisi.

“Tumeambiwa jeshi linaendelea na uchunguzi na hivi tayari wamesha mhoji na kuchukua alama za vidole,” alisema Mkina alipozungumza na Sauti ya Amerika.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:28 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Aidha, vyanzo vya habari vingine vinasema askari hao walivamia ofisi hizo Jumanne mchana wakiwa wamefuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandaona kufanya upekuzi na kuwahoji baadhi ya wafanyakazi.

Baada ya kufanya upekuzi ndani ya ofisi hiyo walielekea nyumbani kwa mkurugenzi huyo, kufanya upekuzi kabla ya kumrudisha rumande kwa vile hakufikishwa mahakamani.

Taarifa iliyotolewa Jumatano na ukurasa huo wa mtandao iliwataka watumiaji wake kutokuwa na hofu yoyote na kwamba Jamii Forums haina mitambo yake mikuu huko Tanzania wala Africa.

"Teknolojia tunayoitumia ya kuficha taarifa (encryption) kumsajili mtumiaji wa JamiiForums.com haituwezeshi kumfahamu mtumiaji yeyote labda yeye akubali kwa hiari yake kujiweka wazi mtandaoni." Ilieleza taarifa hiyo.

XS
SM
MD
LG