Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:31

Trump amteua mkuu wa ExxonMobil kuwa waziri wa mambo ya nje


Mwenyekiti na mtendaji mkuu wa ExxonMobil Rex Tillerson akizungumza wakati wa mkutano wa nishati mjini Houston, Texas April 21, 2015.
Mwenyekiti na mtendaji mkuu wa ExxonMobil Rex Tillerson akizungumza wakati wa mkutano wa nishati mjini Houston, Texas April 21, 2015.

Rais-mteule wa Marekani Donald Trump amemchagua tajiri wa mafuta wa Texas kuwa waziri wake wa mambo ya nje, ikiwa nafasi ya juu katika baraza la mawaziri.

Rex Tillerson, mwenyekiti na mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta ya ExxonMobil hana ujuzi wowote wa kidiplomasia lakini ana uhusiano mkubwa wa biashara katika nchi nyingi za dunia hasa Rashia

Hii ni katika mlolongo wa uteuzi usio wa kawaida ambao Trump amefanya katika kuunda baraza lake la mawaziri. Tillerson akiwa hana uzoefu wowote wa kidiplomasia na uhusiano wake wa karibu na Urusi ni vitu ambavyo wengi wamevikosoa na kusema ni ubinafsi. Bila shaka waziri huyu atakabiliwa na maswali magumu wakati wa mchakato wa kumthibitisha katika Baraza la Seneta ya Marekani.

Rex Tillerson akikula kiuapu kabla ya kutoa ushahidi bungeni.
Rex Tillerson akikula kiuapu kabla ya kutoa ushahidi bungeni.

Uzoefu wa Tillerson katika secta ya mafuta

Tillerson, mwenye umri wa miaka 64, ni mhandisi wa majengo na amejiunga na Exxon baada tu ya kufuzu masomo yake kutoka Chuo Kikuu cha Texas huko Austin na alipanda katika nyadhifa mbali mbali za kampuni hiyo katika kipindi cha miaka 41. Alikuwa tayari kustaafu mwaka ujao kwani angefikia umri wa kustaafu kwa lazima ambao ni miaka 65.

Hata hivyo anajulikana kwa ujuzi wake wa kutengeneza mikataba ya kibiashara ya kimataifa na inasemekana ana uhusiano mazuri na viongozi wa nchi mbali mbali duniani, kitu ambacho kitakuwa ni hazina kubwa kwa mwanadiplomasia wa juu wa Marekani.

ExxonMobil ni kampuni kuu ya tano kwa ukubwa duniani, ukizingatia uwekezaji katika masoko ya kimataifa. Japokuwa kipato cha kampuni hiyo kilipungua kwa kiwango fulani katika miaka ya nyuma kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta duniani, lakini bado ni lenye kutengeneza faida kubwa.

Tillerson, ambae marupurupu yake yanategemea na utendaji wa shirika, aliweza kujiingizia Dola za Kimarekani milioni 27 mwaka jana, kiwango kilichoshuka ukilinganisha na dola milioni 40 mwaka 2012.

Uteuzi wake unaweza kuwa na changamoto

Itabidi Tillerson, athibitishwe na Baraza la Seneti, na inatarajiwa atakabiliana na utata katika machakato huo. Kutokana na uwiano wa sasa wa Seneti, iwapo wademokrat wote watapiga kura kwa kauli moja na warepublikan zaidi ya wawili wakaungana nao, uteuzi warais utakataliwa.

Taarifa ziliendelea kumiminika Jumamosi kwamba Trump alikuwa ameshafanya uamuzi juu ya CEO huyo, maseneta- wakiwemo baadhi ya warepublican- walieleza masikitiko yao juu ya uteuzi wa Tillerson ambae anaushirikiano wa karibu na Urusi.

Rais wa Rashia Vladimir Putin mwaka 2013 alimtunukia nishani ya Urafiki mwema Tillerson, ambae amesimamia mikataba mikubwa ya ExxonMobil na makampuni ya Rashia katika uchimbaji na uzalishaji wa mafuta na gesi na imekeuka vikwazo vya uchumi vilivyowekwa dhidi ya Moscow na serikali ya Washington.

Waziri Mkuu wa Rashia Vladimir Putin, kulia, na Rex Tillerson, na mkuu wa ExxonMobil wakizumgumza kwa faragha mjini Sochi, Russia, Jumanne, Aug. 30, 2011
Waziri Mkuu wa Rashia Vladimir Putin, kulia, na Rex Tillerson, na mkuu wa ExxonMobil wakizumgumza kwa faragha mjini Sochi, Russia, Jumanne, Aug. 30, 2011

Kremlin Jumatatu ilimpongeza Tillerson, kwa kumwita mtu mwenye “weledi mkubwa” katika kazi yake.

David Hamre, rais wa Kituo cha Mikakati na Utafiti wa Kimataifa anasema kuwa Tillerson, ambae pia in mkurugenzi wa bodi ya CSIS, “aliendelea kuwa na ushirikiano na Vladimir Putin kuliko pengine Mmarekani yoyote ispokuwa Henry Kissinger.”

Akizungumza mapema mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Texas, Tillerson alikiri, “Nina uhusiano wa Karibu,” na Putin, kwa kuwa nimekuwa najuana na kiongozi wa Rashia kwa zaidi ya miaka 15.

Uhusiano huo “ndiyo unatia wasiwasi” alisema Seneta John McCain, mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Kijeshi Jumapili.

Maseneta wengine wa Republican, akiwemo Lindsey Graham and Marco Rubio, walieleza kukerwa na uhusiano kati ya Tillerson na Rashia.

Wakati huo huo Seneta wa chama cha Demokrat Robert Menendez amesema kuwa Tillerson kama mwanadiplomasia wa juu wa Marekani, “ utawala wa Trump utakuwa ukiihakikishia Rashia inamtu wao katika maovu yao kwenye Baraza la Mawaziri la Rais-mteule ambae anaongoza sera ya nje ya taifa letu.”

Kulinganisha weledi wa biashara na uzoefu wa kidiplomasia

Wakati baadhi ya wapinzani wanadodosa sifa za Tillerson katika wadhifa huo wa kidiplomasia, Trump amesema katika mahojiano Jumapili kwamba mahusiano ya kibiashara ya kimataifa aliyoyatengeneza Tillerson ndio yanayo mfanya awe ni mtendaji numbari moja wa kimatiafa.

“Amesema anawajua wengi katika watendaji, na anawajua vizuri sana,” Trump alisema.

Rex Tillerson,kushoto, mwenyekiti wa ExxonMobil akikutana na Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji mjini Maputo
Rex Tillerson,kushoto, mwenyekiti wa ExxonMobil akikutana na Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji mjini Maputo

Hata hivyo Profesa Henry Hale, Mtaalamu wa masula ya ulaya na asia katika chuo kikuu cha Washington University ameiambia VOA kuwa “kufanya biashara ugenini sio sawa sawa na kufanya biashara ya kimataifa nje ya nchi.” Lakini akasema kuwa mawaziri wote wa nje wanajifunza kazi hiyo kwa kiwango fulani wakishachukua madaraka.

Uteuzi wa Tillerson unakwenda sambasamba na muelekeo wa Trump juu ya kuwa na wanajeshi na wafanyabiashara katika Baraza lake la Mawaziri.

XS
SM
MD
LG