Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:18

Clinton: Habari feki” ni tishio kwa Demokrasia ya Marekani

Waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton akizungumza katika tafrija ya kumaga kiongozi wa Wademokrats katika baraza la senate Harry Reid, Dec. 8, 2016, in Washington.
Waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton akizungumza katika tafrija ya kumaga kiongozi wa Wademokrats katika baraza la senate Harry Reid, Dec. 8, 2016, in Washington.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, mgombea kiti cha rais Hillary Clinton amesema “habari feki” ni tishio ambalo lazima lishughulikiwe haraka.

Aliyasema hayo wakati wa tafrija siku ya Alhamisi, kumwaga kiongozi wa Wademokrat katika Baraza la Seneta, anaestahafu Harry Reid, ikiwa nimwezi mmoja baada ya kushindwa uchaguzi wa rais, katika kampeni zilizoghubikwa na propaganda na habari za uwongo.

“Ni lazima tusimame kuilinda demokrasia yetu”, alisema Clinton alipokua anataja kile alichokieleza ni, “kuripuka kwa janga la habari feki za kudhalilisha na propaganda za uongo kwenye mitandao ya kijamii kwa mwaka mzima uliopita ni hatari kwa maisha yetu.”

Clinton alihimiza kuwa pande zote; secta binafsi na za umma zinafaa kuichukue hatua za dhati kukabiliana na “habari feki”.

“Sasa ni dhahiri kwamba kile kinachoitwa habari feki kinaweza kuwa na athari mbaya duniani. Hii sio kuhusu siasa au ukereketwa. Maisha ya watu yako hatarini. Maisha ya watu wa kawaida ambao wanataka kuendelea na shughuli zao za kila siku, kufanya kazi zao na kuchangia katika jamii zao,” alisema.

Clinton yeye binafsi amekuwa muathiriwa wa habari fek, ambapo internet ilitumika kuweka madai kwamba Comet Ping Pong, ambayo ni mgahawa unaouza pizza Washington, ulikuwa unasaidia mtandao wa ngono ya watoto inayoendeshwa na Clinton.

Wapita njia wakiweka mauwa mbele ya mgahawa wa Comet Ping Pong pizza
Wapita njia wakiweka mauwa mbele ya mgahawa wa Comet Ping Pong pizza

Kujitokeza Clinton katika tafrija ya Alhamisi, ambayo ilihudhuriwa na viongozi wateule wa Chama cha Democrat; akiwemo Makamu wa Rais Joe Biden, ulishangiliwa kwa shangwe kubwa.

Clinton, ambaye pia ni seneta wa zamani ambae aliwahi kufanya kazi na Reid, alifanya mzaha juu ya kutoonekana kwake na ukimya wake tangu Kiongozi wa Republican Donald Trump aliposhinda uchaguzi Nov 9, akitania kwamba zilikuwa ni wiki chache za kuchukua Selfies (picha za kujipiga mwenyewe kwa simu), vichakani.

Alikiri kwa namna fulani kushindwa kwake alipoanza kutoa sifa na pongezi kwa Ried aliposema, “hii sio hotuba niliyotarajia kutoa hapa Capitol baada ya uchaguzi.”

Sen.Harry Reid, D-Nev. pamoja na Hillary Clinton wakizindua picha ya Ried bungeni

XS
SM
MD
LG