Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 02:50

UM: Rushwa pingamizi kuu la maendeleo, amani na usalama


Maandamano dhidi ya Rushwa Haiti
Maandamano dhidi ya Rushwa Haiti

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha mkataba wa kupambana na rushwa Oktoba 31, 2003, na kutangaza Disemba 9 kua Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Rushwa. Lengo la siku hiyo ni kuhamasisha watu juu ya jukumu la mkataba huo katika kupambana na kuzuia janga hilo. Mkataba ulianza kutekelezwa Disemba 2005.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "tuungane dhidi ya ufisadi kwa ajili ya kuleta maendeleo, amani na usalama."

Sherehe mbali mbali zikifanyika kote dunaini kuadhimisha siku hii kwa kuzungumzia na kuhamasisha watu juu ya athari za ufisadi na rushwa katika maisha ya kila siku ya watu wa kawaida.

Kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa kila mwaka Dola trilioni 1 za Marekani zinatolewa kama rushwa wakati inakadiriwa dola trilioni 2.6 zinaibiwa kupitia ufisadi ambazo ni sawa na zaidi ya asilimia 5 ya pato la taifa (GDP) la dunia nzima.

Misingi ya kupambana na ufisadi

Serikali, sekta za binafsi, asasi za kiraia, vyombo vya habari na wananchi wanashirikiana Disemba 9,duniani kote kupigana na ufisadi. Kama kawaida Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP na lile la kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu,UNODC wako katika mstari wa mbele katika juhudi hizi.

Kwa mujibu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matiafa vita dhidi ya ufisadi ni kero la kimataifa kwa sababu ufisadi ni kitu kinachoendelea kuwepo katika nchi tajiri na nchi maskini.

Mfanyakazi akiripoti rushwa katika ofisi moja Papua New Guinea
Mfanyakazi akiripoti rushwa katika ofisi moja Papua New Guinea

Utafiti ulofanywa na Umoja wa Mataifa, unaonesha kuna ushahidi kwamba ufisadi unawaathiri watu maskini kwa kiwango kikubwa na kuchangia kwa hali ya ukosefu wa Amani, umaskini na ni sababu kuu ya kupelekea nchi kutetereka na kufikia hali ya kushindwa kuwa na utawala wa sheria.

Katika nchi zinazoendelea, kwa mujibu wa taarifa ya UNDP, fedha zinazopotea kupitia rushwa zinakadiriwa kuwa mara kumi ya misaada rasmi ya maendeleo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa, inaeleza kwamba juhudi za kimataifa katika kampeni ya 2016 inalenga kutokomeza ufisadi kwani ni moja ya vikwazo vikubwa katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu ( SDGs).

Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika kuadhimisha Siku ya Kupambana na rushwa kimatiafa (IACD) mwaka huu, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Dawa za kulevya na Uhalifu UNODC imeandaa aina mbali mbali za campaign zinazolenga SDGs na kuainisha ni kwa sababu gani utokomezaji wa ufisadi ni muhimu katika kufikia malengo hayo.

Maadhimisho ya siku ya ufisadi Kenya

Wakenya wanaadhimisha kampeni ya kupambana na rushwa siku mbili tu baada ya Baraza la Kitaifa la Makanisa NCCK kutoa wito kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini humo ivunjwe kwa tuhuma za kuwa imekuwa moja ya vizingiti na udanganyifu mkubwa katika kupambana na ufisadi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kongamano lililofanyika Ukumbi wa Makongamano jijini Nairobi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kutokomeza ufisadi katika taifa la Kenya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa VOA Nairobi Kennedy Wandera siku baada ya siku Rais Kenyatta amekuwa akishutumiwa kuwa hatua ya serikali yake kupambana na ufisadi haziridhishi na kwamba zimeendelea kukwamisha juhudi za kuleta maendeleo nchini.

Wakazi wa Nairobi wanalalamika kwamba rushwa imeota mizizi katika maisha ya kawaida ya watu wote nan i janga kubwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:17 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwanaharakati wa kupambana na rushwa kenyaJohn Githongo akihutubia kongamano la kuadhimisha Siku ya Kupambana na Rushwa Duniani mjini Nairobi, amepongeza hatua za baadhi ya viongozi wa kidini wa Kenya kwa ujasiri wao wa kuwakosoa viogozi wa dini wanaotumia siasa za udini na kuwakatalia kuwahutubia waumini kanisani.

Wanasiasa wa Uganda walaumiwa kuwapora wananchi

Wanaharakati wa kupambana na ufisadi wa Uganda wanataka wanasiasa kutochukulia visa vya ufisadi kama ngao ya kujiimarisha kisiasa dhidi ya wapinzani wao wakisema siasa zimedoofisha vita dhidi ya ufisadi.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kampala Kennes Bwire anaripoti kwamba wanasiasa wanalaumiwa kwa kupora mali ya umma na kujitajirisha kupita kiasi.

Naibu mkurugenzi wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali George Bamugemereire, amewalaumu wanasiasa kuchochea zaidi ulaji rushwa huko Afrika Mashariki akisema mkondo mpya unaotumiwa hii leo ni kwa watu wenye ushawishi mkubwa katika serikali kuwatumia watu wadogo kuiba mali ya umaa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Anawalaumu raia kwa kukosa kufuatilia miradi ya maendeleo na utekelezaji wake, akiongezea kwamba rasilmali za serikali huibwa na wanasiasa baada ya bajeti kuu kusomwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wito unatolewa kwa wananchi kushiriki kikamilifu kuhakikisha miradi inatekelezwa kama inavyoagiziwa na bajeti ya matumizi ya serikali na kuwafichua wezi wa mali ya umaa.

XS
SM
MD
LG