Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 12:26

Magufuli aamuru wamachinga wasibughudhiwe


Rais Magufuli awatetea wamachinga
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:46 0:00

Kukosekana kwa maeneo rasmi ya kufanya biashara ndogo ndogo pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kuhamishwa katika maeneo waliyopewa wawekezaji wakubwa Tanzania tayari kumezusha migongano ya mara kwa mara na kusababisha uvunjifu wa Amani katika maeneo mbali mbali nchini.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali ya kuondoa wafanyabiashara wadogo na wachimbaji wadogo wa madini katika maeneo yanayodaiwa hayaruhusiwi hususan kwenye miji mikubwa kama Mwanza, Shinyanga na Dar es salaam na kuzusha vilio na simanzi baada ya mamlaka husika kwenye miji hiyo kuwaondoa kwa nguvu na kusababisha hasara ya mali zao.

Wiki hii jambo hilo limechukua sura mpya baada ya Rais John magufuli kumuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga katika maeneo yao mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Harakati za sikukuu katika soko la Kariako
Harakati za sikukuu katika soko la Kariako
Wamachinga watafutiwe maeneo rafiki alisema rais Magufuli.


Kufuatia maagizo hayo ya Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa,wilaya na mamamlaka ya serikali za mitaa kuwatafutia wamachinga maeneo rafiki ya kufanyia baishara badala ya kuwabughudhi kwa kuwaondoa katika maeneo yao wanayofanyia biashara na kuwaingizia kipato.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema maagizo yake hayana maana kuwa Wamachinga na Wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sharia. Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.

“Sipendi Wamachinga wafanye biashara kwenye hifadhi ya barabara lakini hakuna sharia katika nchi hii inayosema mtu wa biashara ndogondogo au Mmachinga hatakiwi kukaa katikati ya mji, tukianza kwenda utaratibu wa namna hiyo maana yake tunaanza kutengeneza madaraja ya Watanzania, kwamba kuna Watanzania Fulani wa daraja Fulani wanapaswa kukaa katikati ya mji na Watanzania wa daraja Fulani hawatakiwi kukaa katikati ya mji, huo sio mwelekeo wetu na wala Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo mimi na wewe (Makamu wa Rais) tulipita kuinadi, haisemi tutengeneze madaraja ya watu wanaostahili kukaa mjini na wengine hawastahili kukaa mjini, sasa nimeona hili nilizungumze na nataka kulirudia kwa mara ya mwisho,” amesema Rais Magufuli.

Wananchi katika soko la Kariako kabla ya Eid el Fitr
Wananchi katika soko la Kariako kabla ya Eid el Fitr

Wakati huo huo, Rais pia ameagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyaligongo kilichopo katika Kata ya Mwakitolyo Mkoani Shinyanga na badala yake wachimbaji hao waachwe waendelee na shughuli zao, na leseni ya mwekezaji anayedai eneo hilo ni lake iondolewe.

XS
SM
MD
LG