Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 10:31

Trump athibitishiwa ushindi Michigan


Maafisa katika jimbo la Marekani, la kaskazini la Michigan, wamethibitisha mrepublikan, Donald Trump ndiye mshindi wa urais katika jimbo hilo.

Trump alimshinda mdemokrat Hillary Clinton kwa idadi ndogo ya kura 10,704 kati ya kura milioni 4 zilizopigwa.

Tangazo la Jumatatu limemtangaza rasmi rais mteule kuwa ndiyeo atakayepata kura 16 za wajumbe wa jimbo hilo.

Lakini majimbo mengine mawili ambako uchaguzi ulikuwa wa karibu sana, Pennsylvania na Winsconsin bado yanakabiliwa na kuhesabu tena kura.

Mgombea wa chama cha Kijani Jill Stein tayari amewasilisha malalamiko huko Pennyslvania na Wisconsin na kusema atafanya hivyo hivyo Michigan.

Stein anasema siyo kwamba anajaribu kubadilisha matokeo lakini anataka ukaguzi wa mara ya pili ufanyike katika majimbo hayo ambako matokeo yalikuwa ya karibu sana.

Stein amechangisha mamilioni ya dola kusaidia kulipia zoezi la kuhesabu tena kura.

Lakini hakuna ushahidi wa kusambaa kwa wizi wa kura au kwamba mashine za kupigia kura ziliingiliwa na wahalifu wa mitandao.

XS
SM
MD
LG