Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:59

Maandalizi ya upigaji kura yashika kasi Ghana

Mabango ya kampeni za uchaguzi yakiwa katika mitaa Ghana
Mabango ya kampeni za uchaguzi yakiwa katika mitaa Ghana

Uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura utakamilika mapema wiki ijayo katika kujiandaa na uchaguzi mwezi Desemba , hiyo ni kwa mujibu wa Eric Dzakpasu msemaji wa tume ya uchaguzi ya Ghana .

Tume ya uchaguzi nchini Ghana imesema maafisa wa usalama , waandishi wa habari na maafisa wa tume hiyo, ambao watafanya kazi katika siku ya uchaguzi Desemba wanatakiwa kushiriki katika zoezi maalumu la upigaji kura wiki moja kabla ya nchi nzima kupiga kura.

Uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura utakamilika mapema wiki ijayo katika kujiandaa na uchaguzi mwezi Desemba , hiyo ni kwa mujibu wa Eric Dzakpasu msemaji wa tume ya uchaguzi ya Ghana .

Anasema "tumeanza kuchapisha makarati ya kupigia kura jumapili iliyopita na tunatarajia kukamilisha zoezi hilo Jumapili hii au Jumatatu". Anasema iliwachukua takriban wiki mbili kuchapisha makaratasi ya kura kwa ajili ya wabunge katika majimbo 275 .

Lakini uchapishaji wa karatasi kwa ajili ya kura za urais ni tofauti kidogo kwa sababu inachapishwa aina moja tu ya karatasi yenye muundo mmoja.

XS
SM
MD
LG