Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:15

FBI yafunga uchunguzi wa barua pepe za Hillary Clinton


Mkurugenzi wa FBI James Comey siku ya Jumapili alitangaza kuwa idara hiyo imefunga uchunguzi wa barua pepe za Hillary Clinton.
Mkurugenzi wa FBI James Comey siku ya Jumapili alitangaza kuwa idara hiyo imefunga uchunguzi wa barua pepe za Hillary Clinton.

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi ya Marekani, FBI, aliiandikia barua Congress siku ya Jumapili na kuwaarifu wabunge kuwa baada ya kukagua barua pepe zilizokuwa kwa tarakilishi ya mbunge wa zamani wa New York, Anthony Weiner, shirika hilo limefikia uamuzi wa kutomfungulia mashtaka waziri wa zamani wa mambo ya nje, Hillary Clinton, ambaye amekuwa akituhumiwa kwa matumizi ya mfumo binafsi wa kielektroniki kutuma na kupokea barua pepe za serikali.

Mkurugenzi James Comey alisema kuwa baada ya kufanya uchunguzi usiku na mchana, FBI haikupata ushahidi wowote mpya, na hivyo basi kugunduliwa kwa barua hizo hakutabadilisha msimamo wa idara hiyo kwamba mgombea huyo wa urais kwa chama cha Demokratik, hatafunguliwa mashtaka.

Kampeni ya Hillary Clinton ilielezea kuridhishwa na uamuzi huo. "Tumefurahi kwamba swala hilo limetatuliwa," alisema msemaji wa Bi Clinton, Jennifer Palmieri, ambaye anasafiri naye kwenye kampeni zake.

Takriban wiki moja iliyopita, Comey aliandikia Congress kuwaelezea kuwa idara yake ilikuwa imegundua barua pepe ambazo huenda zingekuwa na uhusiano na uchunguzi uliofanywa awali kuhusu Bi Clinton kutumia taraklilishi binafsi kutuma na kupokea barua pepe za serikali ambazo zilikuwa na alama ya "siri' au "siri kali."

Trump hakupoteza muda katika kuzungumzia maendeleo hayo katika mikutano yake ya kampeni, ikiwa pamoja na ule alioufanya Phoenix, Arizona.

“Hii ni kadhia kubwa sana ya kisiasa tangu ile ya Watergate, na ni matumaini ya kila mmoja kwamba haki, hatimaye, itapatika kwa njia nzuri, “ alisema Trump.

Wakosoaji wa Clinton wameshikilia kwamba hatua hiyo ya Bi Clinton ingehatarisha usalama wa taifa.

​
XS
SM
MD
LG