Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:51

UN: dhuluma na unyanyasaji wa watoto wa kike unaongezeka


Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Mombasa 2016
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Mombasa 2016

Idara ya wanawake ya Umoja wa Matifa UNEFEM inaeleza kwamba mimba na ndoa za utotoni zina athiri ukuwaji wa mtoto wa kike na kuwaondolea ndoto zao za kupata elimu na maisha bora.

Dunia ikisherehkea siku ya mtoto wa kike duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema ustawi, haki za binadamu elimu na kuwawezesha watoto wakike bilioni 1.1 duniani ni nguzo muhimu katika kufikia ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG.

Katika taarifa yake, Bw. Ban ameto wito wa kila mtu kukomesha ubaguzi, dhulma na ghasia dhidi ya wasichana pamoja na kutokomeza mila ya ndoa ya utotoni.

Taarifa anasema inabidi kuahidi kwamba hakuna anaeachwa nyuma, kwani kwa kawaida vijijini, viunga vya miji mkuu na kambi za wakimbizi watoto wakike huachwa nyuma bila ya chakula, huduma za afya au elimu inayostahiki, na kukabiliwa na hatari ya kushambuliwa kingono.

Wanafunzi wa kike wahudhuria sherehe za siku ya mtoto wa kike
Wanafunzi wa kike wahudhuria sherehe za siku ya mtoto wa kike

Huko Tanzania, mkoa wa Shinyanga umetajwa kua na idadi kubwa ya mimba na ndoa za utotoni ambako sherehe za kitaifa zilifanyiika siku ya Jumanne October 11.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha azimio hapo Disemba 19 2011, kutangaza kwamba kila Oktoba 11 itakua ni "Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike" .

Lengo la siku hiyo niu kuhamasisha na kuzingatia haja ya kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto wa kike na kutekeleza haki zao za kibinadam.

XS
SM
MD
LG