Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:22

Al-Shabab yaua watu sita Mandera, Kenya


Map of Mandera, Kenya
Map of Mandera, Kenya

Gavana wa jimbo la Mandera nchini Kenya, Ali Roba, amethibitisha kuwa watu sita wameuawa na mmoja kupata majeraha mabaya baada ya watu waliokuwa wamejihami na wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi la Al-Shabaab, kushambulia jingo la makazi katika mji wa Mandera karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Kwa mujibu wa ujumbe aliouandika katika ukurasa wa Twitter, Roba alielezea masikitikao yake na kuzifariji familia za waliopoteza maisha yao. ”Vifo sita ni vingi mno," alisema kwenye ujumbe huo.

Gavana huyo alisema kuwa maafisa wa usalama walijibu shambulio hilo na kuweza kuwaokoa watu 27, ikiwa ni pamoja na mtu aliyejeruhiwa, kutoka jingo hilo.

Mkazi mmoja wa mji wa Mandera amesema kuwa nyumba iliyoshambuliwa inamilikiwa na wizara ya wafanyakazi ya Kenya na kwamba wengi waliokuwemo ni wafanyakazi wa serikali na wanakandarasi waliokuwa wanajenga ua lililozua utata, kwenye mpaka.

XS
SM
MD
LG