Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:59

Watu 52 wauwawa kwa kukanyagwa Ethopia


Watu wakikimbia kutokana na kufyetuliwa gesi ya kutoa machozi na polisi huko Bishoftu Oromiya siku ya Jumapili
Watu wakikimbia kutokana na kufyetuliwa gesi ya kutoa machozi na polisi huko Bishoftu Oromiya siku ya Jumapili

Waziri mkuu wa Ethopia Hailemariam Desalegn, akanusha kuhusika kwa maafisa wa usalama katika ghasia zilizosababisha vifo vya takriban watu 52 katika jimbo la Oromiya siku ya Jumapili.

Taarifa ya waziri mkuu inaeleza kwamba, upinzani waliwapeleka watu wao kabla ya sherehe hizo kuanza katika mji wa Bishoftu kilomita 40 kusini mwa Addis Abeba, katika lengo la kuvuruga sherehe hizo zinazojulikana kama Irrecha, kando ya mto Harsadi.

watu walojeruhiwa wakati wa ghasia mjini Bishooftuu, Oromiyaa, 2016
watu walojeruhiwa wakati wa ghasia mjini Bishooftuu, Oromiyaa, 2016

Waziri mkuu anaendelea kueleza kwamba, mara shrehe zilipoanza wanaharakati wa upinzani walianzish ghasia na kusababisha umati wa wageni walofika kukimbia na kusababisha watu kukanyagana.

Mashahidi walozungumza na Sauti ya Amerika hata hivyo wanatoa maelezo tofauti kabisa waklisema ghasia zilianza pale wakuu wa serikali walitaka wajumbe wake kuhutubia sherhe hizo, na hapo zogo likaanza. na maafisa wa polisi wakafyetua mabomu ya kutoa machozi ili kujaribu kutawanya watu.

Matokeo yake mashahidi pamoja na viongozi wa upinzani wanasema watu walianza kukimbia kwa hofu na wengine kukanyagwa. Upinzani unadai kwamba huwenda karibu watu 100 walifariki.

watu wakiimba kutaka uhuru zaidi wakati wa sherehe za Irreechaa mjini Bishooftuu
watu wakiimba kutaka uhuru zaidi wakati wa sherehe za Irreechaa mjini Bishooftuu

Tangu mweishoni mwa mwaka 2015 kumekuwepo na maandamano na ghasia katika jimbo hilo la Oromiya ambako idadi kadhaa ya watu wameuliwa kutokana na watu kudai uhuru zaidi wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG