Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:27

Obama afungua Jumba la Makumbusho la Wamarekani wenye asili ya Kiafrika


Rais Barack Obama akizungumza wakati wa kufungua Jumba la makumbushop la historia ya wamarekani wenye asili ya Kiafrika
Rais Barack Obama akizungumza wakati wa kufungua Jumba la makumbushop la historia ya wamarekani wenye asili ya Kiafrika

Rais Barack Obama amefungua rasmi jumba la kwanza la makumbusho la historia na utamaduni wa Wamarekani wenye asili ya kiafrika.

Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa jumba hilo mjini Washington siku ya Jumamosi kwenye uwanja mashuhuru wa “The Mall”, wenye majumbe mengine ya makumbusho kuhusiana na historia ya Marekani, Rais Obama anasema maonesho na hadithi ndani ya jumba hilo, hatimae zitatoa nafasi ya kuwaelimisha wamarekani wote wa kila tabaka, ili kuweza kufahamu sehemu moja ya historia muhimu ya watu weusi.

Rais Obama na Michelle wakimpongeza rais wa zamani Bush
Rais Obama na Michelle wakimpongeza rais wa zamani Bush

“Kama binadamu tumekua tukitoa hadithi na vitandawili vya watu mashuhuri na mabingwa walojenga nchi hii, lakini mara nyingi kwa makusdi au bila ya kupendelea tuajaribu kupamba ile haditi au kupuzi maelezo muhimu ya mamilioni na mamilioni ya wengine. Na kutokana na hayo tunatoa picha isiyo sahihi. Basi hadithi ndani ya jumba hili zitaweza kueleza ukweli wa matukio na historia ya watu wetu kwa ukweli kabisa.”

Ujenzi wa jumba hilo ulogharimu dola milioni 540 ulianza baada ya rais wa zamani George bush miaka 13 iliyopita kutia sainisheria iliyoruhusu bunge la Marekani kugharimia angalau nusu ya gharama za ujenzi.

Jengo la jumba la makumbusho la historia na utamaduni wa wamarekani weusi.
Jengo la jumba la makumbusho la historia na utamaduni wa wamarekani weusi.

Bush aliyehutubia karibu watu elfu saba walohudhuria sherehe za ufunguzi kwamba amefurahi hatimae jingo limejenga mahala inapostahili.

“jumba hili la makumbusho linaonegza sehemu muhimu ya historia ya nchi yetu kwa sababu mbali mbali. Lakini kwanza kabisa inaonesha dhamira yetu ya kujua ukweli. Taifa kuu halifichi historia yake. Hukabiliana na kasoro zake na kuzirekebiosha.” alisema Bush.

Mamia ya wasani na viongozi wa Marekani walihudhuria sherehe hizo ambazo zinaendelea kwa siku mbili kwa tamasha la muziki na maonesho ya utamaduni ndani na nje ya jengo hilo.

Wageni wanaohudhuria tamasha la kusherekea ufunguzi wa jumba la makumbusho la Mmarekani mweusi
Wageni wanaohudhuria tamasha la kusherekea ufunguzi wa jumba la makumbusho la Mmarekani mweusi

XS
SM
MD
LG