Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:34

Mlipuko wasababisha watu 29 kujeruhiwa New York


Polisi wakiwasili kwenye eneo la mlipuko katika mtaa wa Chelsea, Manhattan, jijini New York.
Polisi wakiwasili kwenye eneo la mlipuko katika mtaa wa Chelsea, Manhattan, jijini New York.

Meya wa jiji la New York, Bill de Blasio anasema watu 29 wamejeruhiwa Jumamosi usiku katika mji wa New York kutokana na mlipuko ambao haujulikani unatokana na nini.

Akizungumza na waandishi habari meya de Blasio, anasema uchunguzi unaendelea kutokana na mlipuko huo na polisi wamegundua mlipuko mwengine katika mtaa usio mbali na mahala mlipuko wa kwanza ulitokea.

Wahudumu wa kwanza wakiwasaidia walojeruhiwa
Wahudumu wa kwanza wakiwasaidia walojeruhiwa

Kamishna mkuu wa polisi wa New York James O'Neal akiwa pamoja na meya de Blasio ametoa wito kwa mtu yeyote aliyeshuhudia au kurikodi mlipuko ulipotokea aripoti kwa maafisa husika mara moja.

Amesema mlipuko huo wanaamini ulitegwa kwa makusudi, lakini hawana ushahidi kwamba unahusiana na ugaidi, lakini wanafanya uchunguzi wa kina pamoja na idara za ujasusi za Marekani.

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik Hillary Clinton amezungumza na waandishi habari na kusema wanafuatilia kwa karibu na makini uchunguzi unaofanyika.

Rais Barack Obama amearifiwa juu ya tukio hilo na anasubiri habari zaidi kufahamu sababu za mlipuko huo.

XS
SM
MD
LG