Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 03:17

Watu zaidi ya 10 wafariki baada ya tetemeko Tanzania


Sehemu ya juu ya jengo la maduka imeporomoka kutokana na tetemeko la ardhi mjini Bukoba Sept 10, 2016
Sehemu ya juu ya jengo la maduka imeporomoka kutokana na tetemeko la ardhi mjini Bukoba Sept 10, 2016

Mtetemeko wa wastani wa ardhi ulokua na nguvu za 5.7 kipimo cha Richter umesababisha vifo vya watu 10 na zaidi ya 100 kujeruhiwa na mamia wengine kukoseshwa makazi.

Kufuatana na idara ya Jiolojia ya Marekani, kitovu cha mtetemeko huo ni mji wa Nsunga wilaya ya Kagera, katika eneo la ziwa Victoria, na ulitokea karibu kilomita 10 chini ya ardhi.

Mitetemeko inaripotiwa kutokea umbali wa Kampala, Entebe na Bushenyi nchini Uganda na maeneo kadhaa ya Rwanda na magharibi ya Kenya.

Ramani ya eneo la mtetemeko
Ramani ya eneo la mtetemeko

Mwandishi habari wa Channel 10 Tanzania , Mathias Byabato ameimabia Sauti ya Amerika kwamba maafisa wa wilaya hiyo wamewashauri watu walopoteza makazi yao kulala katika shule na kutorydi katika nyumba zao zilzioporomoka.

Uharibifu kamili haujulikana huku waatalamu wakiendelea kufanya uchunguzi na kujaribu kufahamu hasara iliyopatikana kutokana na mtetemeko huo usio wa kawaida huko Tanzania, ingawa hutokea mara kwa mara upande jirani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

XS
SM
MD
LG