Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 17:20

Waziri John Kerry awasili Nairobi


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, yupo Nairobi, Kenya, kwa ziara ya kikazi ya kudumisha amani.

Bwana Kerry atafanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika Mashariki juu ya namna ya kuizuia nchi ya jirani ya Sudan Kusini kutumbukia tena kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Anategemea kukutana na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kabla ya kujiunga na mawaziri hao kwa mazungumzo ya namna ya kuhakikisha amani inadumishwa katika taifa hilo jipya kabisa duniani.

Bwana Kerry amesema watu wa Sudan Kusini wametaabika kwa muda mrefu na kuendelea kutokuwa na uthabiti kumesababisha kuwepo mamilioni ya wakimbizi.

Mgogoro huo umeelezwa na Bwana Kery kuwa umesababisha pia matatizo ya kibinadamu ambayo yamevuka uwezo hata wa jumuiya ya kimataifa jinsi ya kujibu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG