Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 13:09

Marekani yashutumu shambulizi la Somalia


Marekani imekasirishwa na tukio la Jumapili nchini Somalia pale milipuko miwili iliposababisha vifo vya watu 10, na kushutumu mashambulizi hayo kama ya uoga.

Katika taarifa kutoka baraza la usalama wa taifa ambalo humshauri rais Barack Obama, limesema mashambulizi hayo yanania mbaya kwa ustawi wa amani na demokrasia ya Somalia.

Taarifa hiyo imeeleza mashambulizi yaliyolenga vikosi vya usalama vya Puntland, maafisa wa serekali na raia ni jaribio jingine la magaidi kuidhoofisha Somalia kabla ya tukio lake la kihistoria ya kipindicha mpito wa kisiasa kwa ajili ya uwakilishi zaidi.

Marekani imesema inaungana na jumuiya ya kimataifa kupinga vitendovya kikatili kama hivyo.

XS
SM
MD
LG