Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:08

Al-Shabaab inafanya mipango kushambulia Kenya na Ethiopia -IGAD


Viongozi wa IGAD wakutana kujadilia al-Shabab
Viongozi wa IGAD wakutana kujadilia al-Shabab

Shirika la maendeleo ya kikanda la Afrika Mashariki na pembe mwa afrika, lilisema siku ya Jumatatu kuwa kundi la wanamgambo la Al-shabaab lenye makao yake Somalia, linaendelea kupanga njama za kufanya mashambulizi katika nchi kadhaa katika eneo hilo.

Shirika hilo lilisema kuwa kundi hilo la kigaidi limepanuka na kuanzisha vitengo vipya vya kijeshi, ambavyo malengo yao maalum ni kufanya mashambulizi nchini Kenya na hata Ethiopia.

Katika ripoti yake ya kurasa 53 yenye kichwa; “Alshabab kama tishio la usalama wa Kimataifa.” Igad inasema kuwa hata ingawa ngome kubwa za Al Shabaab ziko Somalia, kundi hilo linatambuliwa na lina matumaini ya kupanuka na kuwa na wanachama katika eneo nzima la Afrika Mashariki.

XS
SM
MD
LG