Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 07:55

Zaidi ya 60 wauawa katika shambulizi la hospitali Pakistan


Pakistani civil society activists light candles Peshawar, Pakistan to pay tribute to the victims of a bombing in Quetta, Aug. 8, 2016.
Pakistani civil society activists light candles Peshawar, Pakistan to pay tribute to the victims of a bombing in Quetta, Aug. 8, 2016.

Mlipuko mkubwa wa bomu la mjitoa mhanga uliotokea katika hospitali moja kwenye mji wa Kusini Magharinbi wa Pakistan wa Quetta siku ya Jumatatu, ulisababisha vifo vya zaidi ya watu sitini na kuwajeruhi takriban watu wengine160.

Maafisa wa hospitali hiyo wamesema kuwa takriban dazeni mbili za wale waliojeruhiwa wako katika hali mahututi na kwamba kuna hofu huenda idadi ya waliouawa ikaongezeka. Wengi wa waathiriwa walikuwa mawakili.

Mlipuko huo ulitokea wakati ambapo kundi la mawakili lilikuwa limekusanyika ili kulalamika na kuomboleza kuuawa kwa rais wa chama cha kimkoa cha mawakili , ambapo watu wasiojulikana walianza kufyatua risasi wakiwa kwenye gari. Waandishi wa habari na wapiga picha ambao walikuwa wanakusanya habari kuhusu malalamiko hayo, ni baadhi ya waliouliwa au kujeruhiwa. Tawi lililojitenga na Taliban ya Pakistan limedai kuhusika na shambulio hilo.

XS
SM
MD
LG