Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:18

Trump, Clinton kuzungumzia uchumi wiki hii


Hillary Clinton - Donald Trump
Hillary Clinton - Donald Trump

Swala la uchumi wa Marekani linatarajiwa kupewa kipau mbele katika kampeni za urais wa Marekani wiki hii, wakati wagombea wote wawili watakapotoa hotuba katika mji mmoja, juu ya mipango yao kwa taifa, iwapo watachaguliwa.

Mgombea wa chama cha Republikan Donald Trump atazungumza leo huku yule wa chama cha Demokratic, Hillary Clinton akizungumza siku ya Ijumaa mjini Detroit, jimbo la Michigan, ambao ni mji unaong’ang’ana kiuchumi na ambo ndio unaofahamika kama mji mkuu wa kutengeneza magari hapa Marekani.

Trump amenukuliwa akisema kuwa atakuwa rais mkubwa Zaidi wa kuwapa watu ajira, kuwahi kuumbwa na Mungu, huku Clkinton akisema kwamba sera zake zitabuni nafasi nyingi Zaidi za kazi tangu vita vya pili vya dunia.

XS
SM
MD
LG