Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 12:28

Rais wa Uturuki ataka adhabu ya kifo kurejeshwa


Umati wa watu wakipeperusha bendera ya Uturuki wakati wa mkutano wa Demokrasia ulotayarishwa na rais Tayyip Erdogan a

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku ya Jumapili aliapa kwamba ataendelea kupambana na mtu yeyote au utawala wowote uatakao jaribu kuhujumu serikali yake.

Akuhutubia halaikai ya mamilioni ya watu waliohudhuria mkutano mkubwa mjini Istanbul, Erdogan aliapa vile vile kuwachukulia hatua wale waliohusika na jaribio la kupindua serikali la mwezi uliopita pamoja na wadhamini wao.

Rais huyo alizungumza kutoka kwa jukwa kubwa lilikuwa na urefu wa mita 60 na lililokuwa na bendera kubwa za taifa na mabango makubwa yenye picha za mwanzilishi wa taifa hilo, Mustafa Kemal Ataturk.

Erdogan, ambaye alihutubia mkutano huop akisimama pamoja na viongozi wa vyama vilwili vikuu vya upinzani, alisema kuwa Uturuki itaendelea katika njia ya kutafuta umoja.

Alisema wananchi watawapenda wenzao sio kwa sababu ya vyeo au majina makubwa. Huku akishangiliwa na umati wa watu waliokuwa wanapeperusha bendera, rais huyo alisema angetia saini mswada wowote ambao ungepitishwa na bunge, kurejesha tena adhabu ya kifo, ambayo ilipigwa marufuku mnamo mwaka wa 2004.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG