Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 05:55

Hillary Clinton ateuliwa mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik

Ujumbe wa California unapiga kura zao kwa ajili ya uteuzi wa mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik mjini Philadelphia , Tuesday, July 26, 2016.
Ujumbe wa California unapiga kura zao kwa ajili ya uteuzi wa mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik mjini Philadelphia , Tuesday, July 26, 2016.

Ukurasa mpya wa kihistoria umeandikwa Marekani Jumane jioni, pale wajumbe wa cha Demokratik wanaokutana huko Philadelphia, kumchagua Hillary Rodham Clinton kua mwanamke wa kwanza kugombania kiti cha rais kwa niaba ya chama kikuu cha kisiasa.

Uteuzi huo umefanyika baada ya wajumbe wa majimbo yote 50 kushiriki katika upigaji kura kwa sauti Jumanne jioni, na kura 15 za ujumbe wa Dakota Kusini zilimhakikishia kupata zaidi ya kura 2 383 zinazohitajika ili kuweza kuteuliwa rasmi.

Wajumbe, pamoja na Meya wa New York, Bill de Blasio, washika mabango Clinton alipoteuliwa rasmi mjini Philadelphia, July 26, 2016.
Wajumbe, pamoja na Meya wa New York, Bill de Blasio, washika mabango Clinton alipoteuliwa rasmi mjini Philadelphia, July 26, 2016.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nchi za nje anakua mgombea rasmi wa kiti cha rais pamoja na mgombea mwenza wake Tim Kaine, baada ya mapambano makali na Seneta Bernie Sanders, aliyetangaza rasmi hoja ya wajumbe kumkubali kua mgombea wa chama hicho.

Hivi sasa Clinton atanaza mapambano makali dhidi ya mgombea kiti wa chama cha republikan Donald Trump kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Novemba 8, 2016. Wajumbe walianza kuimba "Hillary, Hillary." baada ya matokeo rasmi kutangazwa.

XS
SM
MD
LG