Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 04:25

Trump azungumzia kuijenga upya Marekani


Kufungwa kwa mkutano mkuu wa chama cha Republican mjini Cleveland, Ohio

Akikubali uteuzi wake kama mgombea rasmi wa kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Republican, Doland Drump amesema Marekani itakua taifa salama mara atakapoapishwa rais hapo Januari 20 mwaka 2017.

Katika hotuba ya zaidi ya saa moja tajiri mfanyabiashara anaeingia katika siasa, amekosoa vikali utawala wa Rais Barack Obama kuanzia kuongezeka kwa uhalifu, uhamiaji, uchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, umaskini hadi uhusiano wa kimataifa.

Donald Trump akitoa hotuba ya kukubali uteuzi wake
Donald Trump akitoa hotuba ya kukubali uteuzi wake

Akimgeukia Hillary Clinton, atakae kua mpinzani wake katika uchaguzi wa rais, Trump amesema utendaji kazi wake kama waziri wa mambo ya nchi za nje imeiwacha nchi katika hali mbaya.

Anasema alipochukua nafasi hiyo hapakuwepo na kundi la ISIS lakini hii leo limeenea kote duniani, akiongeze kua amesababisha ghasia na vita tangu Libya hadi Syria na Iran iko njiani kutengeneza silaha za nuklia.

Katika hotuba yake hiyo ndefu ameahidi kufanya mambo mengi akichukua madaraka lakini hakusema atafanya vipi au kufuata mpango gani au gharama itakayohitajika kuterkeleza mambo hayo yote.

Wajumbe wa nchi za Amerika ya Kati ndani ya ukumbi wa mkutano
Wajumbe wa nchi za Amerika ya Kati ndani ya ukumbi wa mkutano

Wachambuzi wanasema hotuba yake ilikua yenye utulivu kulinganisha na nyenginezo, lakini hakupendekeza lolote juu ya namna ya kukiunganisha chama chake baada ya matukio mbali mbali yaliyotokea wiki hii hapa Cleveland.

Baadhi ya wajumbe walohudhuria mkutano huu wanasena wanaondoka wakiwa hawajaridhika na mambo yaliyotokea na hawana hakika watakua na juhudi zinazohitajika kumsaidia Trump kupata ushindi.

XS
SM
MD
LG