Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:18

Mvutano wazuka kwenye mkutano wa Republican


Ghasia zatokea kwenye siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa chama cha Republican hapo jana baada ya wakuu wa chama kuzuia juhudi za dakika za mwisho za kubadili kanuni za mkutano.

Hoja ya kutaka wajumbe wapewa nafasi ya kuamua nani wanampendelea kumpigia kura badala ya kumchagua mshindi wa uchaguzi wa awali iliwasiloishwa na kundi linalompinda Trump.

Kundi la kumpinga Doland Trump liliongozwa na washirika wa Ted Cruz walowasilisha hoja iliyotiwa saini na wajumbe kadha kutaka kulazimisha kanuni kupitishwa kwa kura ya wajumbe badala ya kura ya sauti.

Kufikia saa kumi jioni kanuni zilipitishwa, licha ya makeleke na fujo kutoka wapinzani. Bill Thomas wa Hampton Virginia anasema hawatakubali kanuni hizo kubadilishwa.

"Wanataka wajumbe kama mimi tuweze kubadili kura yetu kutokana nna imani tuliyonayo badala na matakwa ya wanachama wetu jambo hilo halitowezekana."

Seneta Mike Lee wa utha moja wapo ya viongozi wanaoongoza uwasi wanasema wanataka kubadili kanuni kwaajili ya uchaguzi wa 2020, wakitaka kuwazuaia wagombea kutoka nje kutoweza kugombania kiti cha rais kama alivyofanya Trump mwaka huu. Akisema juhudi ni kwa ajili ya mustakbal wa chama.

Kutokana na uwamuzio huo wajumbe kutopka jimbo la Colarado waliondoka kwenye mkutano na hivi sasa mvutano huo utaendelea pengine hadi mwisho wa mkutano huu. Hivi punde mke wa Trump Melania pamoja na meya wa zamani ewa New York waliwahutubia wajumbe na kuzungumzia jinsi Trump atakavyoimarisha usalama akichaguliwa.

Nje ya mkutano Msani mashuhuri Nick Cannon alijitokeza na wanaharakati wa Black lives matter na kusema hatopiga kura katika uchaguzi wa rais na kuwataka wamarekani weusi kutopiga kura hadi pale wagombea rais waeleze vipi watafanya mageuzi ya mfumo wa sharia na kutilia maanani maisha ya watu weusi.

"Tunazungumzia uchaguzi wa rai, na hakuna kati ya wawili tunaweza kumchagua, hata ikiwa tutamchagua aliye bora kati ya mazimwi wawili, kwa hivyo hadi pale kuna mgombea atakae tueleza mpango wa kubadili mfumo wa sharia na kushughulika masuala yanayotuhusu, tutabaki na msimamo wetu."

Cannon anasema hawashauri watu kutopiga kura bali wapige kura kuwachagua wajumbe watakaowakilisha malengo yao katika viwango vya serikali ya mitaa wilaya na jimbo.

Wachambuzi wanasema mkutano wa Clevelad unaonekana unaelekea kama walivyo tabiri kuwepo na mvutano ndani ya chama na upinzani mkubwa nje ya mkutano

XS
SM
MD
LG