Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:25

Watu 15 wauliwa katika shambulizi la hoteli Mogadishu


 Moshi mkubwa waonekana ukitanda baada ya shambulizi kwenye hoteli ya Naso-Hablod Hotel mjini Mohadishu , June
Moshi mkubwa waonekana ukitanda baada ya shambulizi kwenye hoteli ya Naso-Hablod Hotel mjini Mohadishu , June

Kikosi maalum cha usalama cha Somalia "Al-pha Group" kimefanikiwa kuwashinda nguvu wanamgambo wa al-Shabab walovamia hoteli moja karibu na uwanja wa ndege wav kimataifa wa Mogadishu na kusababisha vifo vya karibu watu 15 na wengine 25 kujeruhiwa.

Msemaji wa wilaya ya Mogadishu Abdifitah Omar Halane ameiambia VOA kwamba, utekaji nyara ulofanyika baada ya wanamgambo wa al-Shabab kushambulia kwa bomu lililotegwa ndani ya gari nje ya hoteli ya Naso-Hablod ulimalizika usiku ya Jumamosi.

Wanamgambo waliwasili mbele ya hoteli wakati wa alasiri ya Jumamosi na mjitoa mhanga mmoja alilipua gari lililojaa milipuko, kabla ya wenzake kushambulia kwa bunduki.

Mwanidshi wa Sauti ya Amerika aliyefika karibu na eneo hilo kaskazini ya uwanja wa ndege wa Mogadishu anasema, kulikuwepo na mapigano makali kabla ya wanamgambo kuingia na kushikilia mateka baadhi ya watu ndani ya hoteli hiyo.

XS
SM
MD
LG