Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:20

Obama asema Marekani ni bora kwa uwekezaji


Rais Obama akizungumza katika mkutano wa uwekezaji
Rais Obama akizungumza katika mkutano wa uwekezaji

Rais wa Marekani Barack Obama amesema hakuna sehemu nzuri zaidi au muda wa kuwekeza kuliko Marekani wakati huu.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema hakuna sehemu nzuri zaidi au muda wa kuwekeza kuliko Marekani wakati huu.

Rais Obama alitoa maelezo hayo mjini Washington Jumatatu katika mkutano wa uwekezaji unaojulikana kama SelectUSA uliojumuisha maafisa waandamizi wa Marekani, wakurugenzi katika sekta ya biashara, na viongozi wengine ukiwa na lengo la kuchochea uwekezaji wa moja kwa moja wa nje ndani ya Marekani.

Katika maelezo yake Obama alisema mkutano huo unatoa fursa kwa kila upande Marekani kwa ajili ya uwekezaji wa dunia. Amesema jumuiya za ndani zinazokaribisha uwekezaji wa nje zinakuwa kwa haraka kiuchumi kuliko zile zinazogomea fursa hiyo.

Anasema kwa sababu mkutano kama huu ulifanyika miaka mitatu iliyopita makampuni yaliyoshiriki yaliwekeza zaidi ya dola bilioni 10 katika majimbo 35 ya Marekani na vitongoji vyake.

Obama amesema mkutano huo hauna lengo tu la kufikia makubaliano ya mikataba na kutengeneza pesa, ajira na biashara lakini pia una lengo la kuweka ushirikiano bora kote katika mipaka. Anasema makampuni yanapokuja pamoja inapelekewa uwelewa mzuri wa watu kutoka katika mipaka na kote duniani.

SelectUSA ni programu ya Serikali inayohusisha biashara kimataifa ndani ya idara ya biashara ya Marekani. Programu hiyo imeripoti kuwa tangu ilipoanzishwa imeweza kuwekeza zaidi ya dola bilioni 19 na kutengeneza maelfu ya ajira Marekani.

XS
SM
MD
LG