Miili ya watu 34, 20 kati yao wakiwa watoto imeokotwa ikisadikiwa walikuwa wakijaribu kuvuka jangwa nchini Niger. Maafisa wa serikali wamesema wanaamini kwamba waathirika walikuwa wahamiaji wanaosafiri kaskazini kwa matumaini ya kufika Algeria au Ulaya.
Wizara ya mambo ya ndani ya Algeria ilitangaza ugunduzi huo Jumatano.Taarifa kwenye televisheni ya taifa imeeleza kwamba wanawake tisa, wanaume watano na watoto 20 walifariki dunia baada ya kutekelezwa kwenye jangwa na wasafirishaji haramu wa binadamu.
Utaifa wa waathirika hao bado haujatambulika .Taasisi ya kimataifa ya Uhamiaji inasema uhamiaji kutoka Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Ulaya umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya Afrika magharibi na kati katika siku za karibuni.