Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 20:07

Rwanda yawarudisha warundi 400 nyumbani


Wakimbizi wa Burundi Rwanda
Wakimbizi wa Burundi Rwanda

Serikali ya Rwanda imeamrisha kurudishwa Burundi karibu warundi 400 ikiwatuhumu kwa kufanya ujasusi na kuchochea mvutano kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika ya Kati.

Uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umezorota kutokana na hali ya kisiasa huko Burundi tangu Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombania madaraka kwa mhula wa tatu mwaka jana.

Mmoja kati ya watu walofukuzwa ni kijana ambae hakutaka jina lake litajwe na amelithibitishia shirika la habari la Reuters kwamba maafisa wanawatuhumu kwa kufanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya Bujumbura.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja ambapo warundi wanafukuzwa kutoka Rwanda kwa sababu mbali mbali na katika kipindi hicho idadi ya walofukuzwa imefikia 1 700.

Maafisa wa Burundi wamethibitisha tukio hilo wanaosema lilitokea Alhamisi na Ijumaa na walofukuzwa waliwasili kupitia wilaya ya Bugabira, kaskazini ya nchi.

XS
SM
MD
LG