Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 06:57

Uganda yakanusha kuwakamata polisi walomlinda Besigye


Polisi wanaoshika zamu wanawazuia waandishi habari kufika karibu na Feb. 22, 2016.

Polisi wapatao 20 wa Uganda walokua zamu kumlinda kiongozi wa upinzani Kiza Besigye, akiwa anashikiliwa nyumbani kwake Kaswangati wamekamatwa na maafisa wa usalama wa nchi hiyo.

Vyanzo vya kuaminika vya polisi mjini Kampala vikizungumza na Sauti ya Amerika, vinaeleza kwamba polisi hao wanashikiliwa na kuhojiwa kuhusu jinsi Dk. Besigye alivyoweza kutroroka kutoka nyumbani kwakena kuhudhuria mkutano na wafuasi wake wiki iliyopita.

Hata hivyo msemaji wa polisi Patick Onyango amekanusha habari hizo siku ya Jumamosi alipozungumza na waandishi habari na kusema hawezi kutoa maelezo zaidi isipokua kusisitiza kua polisi hao hawajakamatwa.

Dr Besigye kwa wakati huu anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Moroto, baada ya kukamatwa pale video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha anakula kiapu kama rais wa wananchi wa Uganda.

Mwendesha mashtaka wa taifa amemfungulia rasmi mashtaka ya uhaini kutokana na kitendo hicho.

XS
SM
MD
LG