Huenda kuchipuka kwa makundi ya kihalifu na kigaidi nchini Kenya kumewaweka maafisa wa polisi nchini humo katika hali ya tahadhari.
Mnamo siku ya Jumapili wiki iliyopita polisi mjini Mombasa nchini Kenya Walisimamisha mkutano ulioandaliwa na vuguvugu moja la viongozi wa kiislamu linalojiita Hizbut Tahirir kutokana na sababu za kiusalama.