Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:22

Kenya yateketeza pembe ili kuzuia mauwaji ya ndovu


Rais Uhuru Kenyatta (Kulia) na mwenzake Ali Bongo Ondimba wa Gabon wakisimama pamoja baada ya kutia moto tani 105 ya pembe za ndovu.
Rais Uhuru Kenyatta (Kulia) na mwenzake Ali Bongo Ondimba wa Gabon wakisimama pamoja baada ya kutia moto tani 105 ya pembe za ndovu.

Moshi mweusi ulitanda kwenye anga za mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Nairobi, baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuchoma tani 105 za pembe za ndovu na tani 1.35 za vifaru siku ya Jumamosi, katika lengo la kuwasilisha ujumbe duniani kwamba itapambana vikali na majangili.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Rais Ali Bongo wa Gabon na wajumbe wa serikali kadhaa za Afrika lilikua la kwanza la aina yake la kuchoma idadi kubwa kabisa ya pembe duniani.

Rais Kenyatta azungumza baada ya kutia moto pembe za ndovu
Rais Kenyatta azungumza baada ya kutia moto pembe za ndovu

Akizungumza baada ya kuchoma moto pembe hizo, Rais Kenyatta alisema urefu wa kila fungu la pembe ni kiwango cha dhamira yao katika kupambana na ujangili.

"Mbele yenu mabwana na mabibi ni kiwango kikubwa kabisa cha pembe kuwahi kuharibiwa kwa namna hii. Na sababu yetu ni wazi na bayana. Hakuna mtu - ninarudia - hakuna mtu ana haja ya kuhusika katika biashara ya pembe, kwa sababu biashara hii inamanisha mauwaji. Mauwaji ya mdovu zetu, urithi wetu wa kitaifa." alisema Rais Kenyatta.

Kenya iliamua kuchoma pembe hizo ili kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuzuia janga la uwindaji haramu ya wanayama pori, unaosababisha mauwaji ya maelfu ya ndovu kote barani Afrika.

Tangazo ka kusitisha biashara haramu ya pembe
Tangazo ka kusitisha biashara haramu ya pembe

Mustakbala wa Tembo na vifaru utatengemea uwezo wa mataifa kupambana na kupiga vita uwindaji haramu wa wanyama pori, hayo yalisemwa siku ya jumamosi na viongozi mbalimbali wa afrika pamoja na wanaharakati wa mazinginga, katika tukio hilo.

Inasadikiwa idadi ya tembo wanaoishi barani Afrika imeshukua kutoka milllion 1.2 katika miaka ya 1970 mpaka kufikia 400,000 kwa wakati huu.

Kati ya mwaka 2010 mpaka 2012 inasadikika zaidi ya tembo 30,000 waliuwaa na kutishia kutoweka kwa wanyama hao wakuu kutoka dunia.

Wakati hali kwa vifaru wanaoishi ni mbaya zaidi kwani wamebaki 30,000, au watapotea kabisa kama uthibiti wa uwindaji haramu hautofatwa.

Kenya yateketeza pembe za ndovu na vifaru
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:33 0:00

XS
SM
MD
LG