Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:54

Malta yazuiya mafuta ya Libya kuingia nchini kwake


Picha ya John Kirby
Picha ya John Kirby

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani John Kirby amesema , Marekani ina wasiwasi kuhusu manunuzi hayo ya mafuta nje ya taratibu sahihi za Libya.

Malta imeizuia meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya India kuingia katika himaya yake ya bahari kwa sababu ilikuwa imebeba mafuta kinyume cha sheria kutoka Libya .

Meli hiyo yenye jina la Distya Ameya ilizuiliwa kutoka umbali wa kilometa 12 kaskazini mashariki mwa ufukwe wa Malta hapo jana. Meli hiyo ilikuwa imebeba mapipa 650,000 ya mafuta ghafi yaliyouzwa na utawala wa Libya mjini Tobruk.

Shirika la habari la Bloomberg linasema mnunuzi wa mafuta hayo ni kampuni iliyopo katika falme za kiarabu.

Utawala wa upinzani wa Tripoli umedai kuwa uuzaji wa mafuta hayo ni kinyume cha sheria na kusema kwa sababu shirika la kitaifa la mafuta ni taasisi pekee nchini humo inayotambulika kimataifa kwamba inaweza kufanya mauzo ya mafuta ya Libya.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani John Kirby amesema , Marekani ina wasiwasi kuhusu manunuzi hayo ya mafuta nje ya taratibu sahihi za Libya.

XS
SM
MD
LG