Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 10:46

Watu 140 wauwawa Sudan Kusini


Brigedia generali Lul Ruai Koang, wa jeshi la Sudan People's Liberation Army huko sudan kusini katika picha, April 14, 2016.

Maafisa wa Ethiopia wamelaumu shambulizi la ijumaa karibu na Gambella linalosadikiwa kufanywa na wanaume wa kabila la Murle

Makundi yenye silaha Sudan Kusini yamefanya operesheni katika mpaka na kuuwa zaidi ya watu 140 na kuteka watoto wengi , serikali ya Ethiopia imesema Jumapili.

Maafisa wa Ethiopia wamelaumu shambulizi la ijumaa karibu na Gambella linalosadikiwa kufanywa na wanaume wa kabila la Murle. Wanasema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliouwawa, na idadi kubwa ya watoto walitekwa na kurejeshwa Sudan Kusini.

Waziri wa habari wa Ethiopia, Getachew Reda ameliambia shirika la habari la kimataifa la Associated Press kuwa Jeshi la kulinda amani la Ethiopia linawasaka wachochezi .

Reda amesema hakuna uhusiano wowote baina ya washambuliaji na Serikali ya Sudan Kusini au waasi nchini humo.

Amesema vikosi vya Ethiopia vimeuwa washambuliaji 60 hadi sasa na wanaweza kwenya Sudan Kusini kuwasaka wapiganaji wenye silaha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG