Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:47

Jamuhuri ya Afrika ya Kati yatangaza baraza la mawaziri


Rais mpya wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Faustine-Archange Touadere ametangaza baraza ake la mawaziri.

Inaelezwa baraza hilo linatoa ubashiri wa juhudi za kufikia muafaka wa nchi yake kufuatia miaka kadhaa ghasia za kupingana.

Toyadera amewataja washirika wake wa kisiasa na wapinzani wake wa zamani katika serikali mpya lakini amewaacha wafuasi wa vikundi vya wanamgambo wa kislamu na kikristo ambao nao wanawajibika katika ghasia za nchi hiyo.

Nafasi tatu za juu katika baraza lenye mawaziri 23 zimekwenda kwa wagombea walioshindana dhidi ya Touadera mwaka huu katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais.

XS
SM
MD
LG