Mrepublican Ted Cruz na Mdemocrat Bernie Sanders, ambao wako nafasi ya pili katika kinyan'ganyiro cha kugombania nafasi ya kuwakilisha vyama vyao, wameleta changamoto mpya katika mashindano hayo kwa kupata ushindi muhimu katiika jimbo la Wisconsin Jumanne usiku.
Cruz amemshinda Donald Trump kwa karibu asili mia 15 kufuatana na matokeo ya awali, na hivyo kupunguza kasi za tajiri huyo na hata kuzusha uwezekano mkubwa kwamba mshinda atachaguliwa kwenye mkutano mkuu wa julai huko Cleveland.
Kwa upande wake mdemocrate Bernie Sanders Seneta kutoka jimbo la Vermont, amemshinda Hillary Clinton kwa asili mia 55 na kumpelekea waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje kutangaza kwamba anabadili mkakati wake ili kuweza kumondowa mpinzani wake kutoka mashindano hayo mapema.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Joel Ulomi huko Huston Texas, anasema hivi viongozi wakuu wa chama cha Republican walotaka kuzuia kasi za Trump wanasherekea kwani Cruz amefanikiwa kufanya hivyo.