Maafisa wa Iraq wanasema shambulizi la kujitoa muhanga Ijumaa usiku limeuwa takriban watu 30 na kujeruhi wengine zaidi ya 80.
Maafisa wa usalama wanasema mshambuliaji alitegua milipuko katika uwanja wa michezo kilomita 40 kusini mwa mji mkuu wa Baghdad.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa shambulikzi lilizuka wakati maafisa walipokuwa wanatoa vikombe vya ushindi kwa wachezaji kwenye mashindano ya mpira wa miguu.
Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulizi hilo.