Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:59

Rais wa Angola atangaza kuachana na siasa mwaka 2018


Rais wa Angola Jose eduardo dos Santos
Rais wa Angola Jose eduardo dos Santos

Akizungumza na viongozi wa chama tawala nchini humo MPLA katika mji mkuu wa Luanda, dos Santos amesema amechukuwa uwamuzi wa kuachana na siasa mwaka 2018.

Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, mmoja wapo wa marais wa Afrika waliokaa madarakani muda mrefu ametangaza hii leo kwamba atang’atuka siasa mwaka 2018 wakati muda wa muhula wake wa sasa unamalizika.

Akizungumza na viongozi wa chama tawala nchini humo MPLA katika mji mkuu wa Luanda, dos Santos amesema amechukuwa uwamuzi wa kuachana na siasa mwaka 2018.

Muhula wa sasa wa rais huyo unamalizika mwezi Semtemba mwakani.

Hakueleza kwa nini atang’atuka mwaka mmoja baadaye, wala sababu za kustaafu kwake.

Dos Santos mwenye umri wa miaka 73 ameiongoza Angola toka mwaka 1979.

Ni Rais wa pili barani Afrika kukaa madarakani akimfuatia Rais Teodoro Obiang Nguema, wa Equatorial Guinea . Wakosoaji wamemshutumu dos Santos kwa kutumia utajiri wa nchi wa mafuta kujinufaisha yeye mwenyewe, familia, na washirika wake.

XS
SM
MD
LG