Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 23:58

Uchaguzi wa Uganda kupingwa mahakamani


Uchaguzi Uganda 2016
Uchaguzi Uganda 2016

Uchaguzi huo uliofanyika mwezi Februari unatarajiwa kupingwa na aliyekuwa mgombea Amama Mbambazi na chama chake akidai kuwa haukuwa wa huru na haki.

Jopo la majaji tisa wakiongozwa na jaji mkuu wa Uganda Bert Katurebe, wataanza kusikiliza rufaa iliyowasilishwa katika mahakama kuu kupinga ushindi wa Yoweri Museveni kama rais wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Februari.
Museveni ametayarisha mawakili 40 huku Mbabazi akiwa na mawakili 43. Mbabazi, anataka matokeo ya kura kufutiliwa mbali na uchaguzi kuandaliwa upya kwa msingi kwamba sheria zote za uchaguzi zilivunjwa na wizi wa kura kutekelezwa.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakati huo huo wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Uganda wamesema ni vyema mvutano na mzozo wa uchaguzi huo kutatuliwa mahakamani.

XS
SM
MD
LG