Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:38

Rais wa Somalia asema wanajeshi wa Kenya wapatao 200 waliuawa


Wanajeshi wa Kenya wakitoa heshima za mwisho kwa wenzao waliouwawa Somalia.
Wanajeshi wa Kenya wakitoa heshima za mwisho kwa wenzao waliouwawa Somalia.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema kati ya wanajeshi 180 na 200 wa Kenya waliuawa wakati wanamgambo wa kiislamu waliposhambulia kituo cha Umoja wa Afrika Kusini Magharibi mwa Somalia mwezi jana.

Mohamud aliyasema hayo wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Somalia Jumatano, alipoulizwa kwa nini alihudhuria sherehe za kumbukumbu ya wanajeshi nchini Kenya.

Wanajeshi wa Kenya wakiwa wamebeba jeneza la mwenzao aliyeuwawa Somalia
Wanajeshi wa Kenya wakiwa wamebeba jeneza la mwenzao aliyeuwawa Somalia

Rais huyo alisema “Wakati vijana kati ya 180 na 200 waliotumwa Somalia kurejesha amani wanapouawa asubuhi moja, hilo si jambo rahisi.”

Lakini msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo haraka alikanusha madai hayo. Akizungumza na gazeti la The Star, Obonyo alisema kwamba idadi aliyoitaja rais huyo ni kubwa mno.

Serikali ya Kenya haijawahi kutoa idadi kamili ya wanajeshi waliouawa wakati wanamgambo wa Alshabaab wapolivamia kambi hiyo iliyo katika mji wa el Adde. Al-Shabaab walidai kuhusika na kusema kwamba waliwaua Zaidi ya wanajeshi 100 wa Kenya.

Wakati huo huo, watu wasiopungua wanne wameuawa Alhamisi baada ya Magaidi wa Alshabaab kufyetua kombora lililolenga makao ya rais wa Somalia lakini badala yake likagonga nyumba jirani ya kibinafsi. Mwandishi wa sauti ya Amerika amesema kwamba mama mmoja na watoto wake wawili walifariki papo hapo, na baadae baba yao alikufa muda mfupi baada ya kukimbizwa hospitalini. Watu wasiopungua watano walijeruhiwa, ingawa serikali haijasema lolote kuhusu shambulio hilo.


XS
SM
MD
LG