Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 16:17

Sanders na Trump washinda katika kinyang'anyiro cha New Hampshire.


Mrepublikan Donald Trump akiwapa busu washabiki wake huko Iowa.Jumatatu Feb.1
Mrepublikan Donald Trump akiwapa busu washabiki wake huko Iowa.Jumatatu Feb.1

Mdemokrat msoshalisti Bernie Sanders na bilionea msemaji Donald Trump wameshinda katika kinyang'anyiro cha uteuzi katika uchaguzi wa awali katika jimbo la New Hampshire wakipata ushindi wao wa kwanza katika kampeni za urais kwa mwaka 2016.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:44 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Muda mfupi baada ya vituo vya kuhesabu kura kufungwa vituo vyote vikuu vya habari viliwatangaza Trump na Sanders washindi. Na katika ushindani mkali wa nafasi ya pili katika chama cha Republikan Gavana wa Ohio John Kasich alimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Donald Trump.

Matokeo haya yalifanana kabisa na matokeo ya hivi karibuni ya kura za maoni ambazo zilionyesha seneta wa Vermiont Bernie Sanders na bilionea wa biashara za nyumba Donald Trump wakiwashinda kwa kiasi kikubwa washindani wenzao katika jimbo hilo la New Hampshire.

XS
SM
MD
LG