Upatikanaji viungo

Mgombea wa urais katika uchaguzi wa Febuari 18 nchini Uganda, Dkt Kiiza Besigye amejibu kauli iliyozua utata iliyotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Siku chache zilizopita Rais Yoweri Museveni alitamka kwamba Uganda ni shamba lake la ndizi na hawezi kuondoka wakati ndizi zinakaribia kukomaa.
Museveni aliongeza kusema kwamba hawezi kumruhusu mtu yeyote kuzivuna ndizi za shambani kwake.
Kufuatia matamshi hayo kiongozi wa chama cha FDC, Dkt Kiiza Besigye, yeye amemlinganisha Rais Museveni na mti mkubwa uliotikiswa sana, mizizi yake kukatika na unaokaribua kuanguka wakati wowote.
Usemi wake Besigye umekaribiana na mgombea mwengine wa urais Amama Mbabazi, ambaye alikuwa mjini Busia, Jumatano na kuwataka wapiga kura katika eneo hilo kumuondoa Museveni madarakani ili kujiendeleza kiuchumi.

Maoni yako

Onyesha maoni

XS
SM
MD
LG