Upatikanaji viungo

Idadi kubwa ya polisi imeonekana kuwafuata wagombea wa urais nchini Uganda Dkt Kiiza Besigye na Amama Mbabazi wapinzani wa Rais Yoweri Museveni.

Taarifa zinadai kila wanakokwenda wagombea hao huwa kuna polisi na kuzuiwa kuingia katika maeneo ya uma kama vile hospitalini na sehemu za ibada.

Inaelezwa hali hiyo inatokana na agizo la tume ya uchaguzi ya Uganda licha ya kutokuwepo sheria kuwazuia wanasiasa kuingia katika sehemu hizo.

Agizo la tume ya uchaguzi limetolewa baada ya Dkt Besigye kuingia katika hospitali iliyo na muuguzi mmoja, bila dawa wala vifaa vya matibabu na kuikejeli serikali ya Rais Museveni kwa kukosa kuwahudumia raia.

Wafuasi wa Dkt Besigye tayari wameonyesha uhasama kwa kufuatwa mgombea wao na idadi hiyo kubwa ya polisi na kuzua majibizano.

Maoni yako

Onyesha maoni

XS
SM
MD
LG