Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:25

Rajabu: Mazungumzo ndio njia ya kusuluhisho mzozo wa Burundi


Maandamano ya kumpinga Nkurunzinza, Burundi
Maandamano ya kumpinga Nkurunzinza, Burundi

Viongozi wa kundi jipya la uwasi la Burundi, Republican Force of Burundi Foreb, wanataka kuwalinda wananchi na mali zao pamoja na kuzuia umwagikaji damu unaoendelea nchini humo, amaesma mwenyekiti wa zamani wa chama tawala cha Burundi Hussein Rajabu.

Akizungumza akiwa uhamishoni Bw Rajabu amethibitisha kwamba kundi hilo linalotokana na mpasuko wa jeshi la taifa liko ndani ya nchi na liko tayari kurudisha demokrasia kwa warundi.

Hussein Rajabu azungumzia ghasia za Burundi
please wait

No media source currently available

0:00 0:12:27 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwanasiasa huyo anasema wanasiasa wote wa Burundi wanaopinga uwamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kugombania muhula wa tatu wako tayari kwa mazungumzo na wanataka majadiliano kwa misingi ya makubaliano ya Arusha.

"Mimi nina kwenda kwa mazungumzo ya Kampala kama mjumbe wa chama cha CNDD-FDD "ambacho kinaheshimu katiba na sheria ya nchi ambayo ni miongoni mwa makundi na vyama vilivyounda vuguvugu na CNRS."

Bw Rajabu anasema njia ya kutanzua mzozo wa kisiasa wa nchi yake ni mazungumzo na amepongeza juhudi za kikanda na kimataifa katika kutafuta amani na kuweka kishinikizo kwa utawala wa Burundi.

XS
SM
MD
LG