Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 23:16

Wakristu Duniani Wanaadhimisha Krismas Leo


Wakristu duniani kote leo hii wanaadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu kwa siku kuu ya Krismas.

Siku hii hutumiwa na Wakristu kwa kufanya ibada pamoja na kujumuika na familia kwa kula na kunywa.

Baba mtakatifu Francis aliongoza waumini bilioni 1.2 wakatoliki katika mkesha wa krismas Alhamisi usiku kwa misa kwenye kanisa la St. Peter’s Basilica.

Katika hotuba yake, baba mtakatifu amekemea ulevi wa jamii katika ulaji, furaha, wingi na utajiri.

Akizungumzia kuzaliwa katika mazingira ya kawaida mno kwa Yesu, Papa Francis amesema Yesu, anatutaka tufuate maneno yake, akimaanisha tuwe na maisha ya kawaida, yenye uwiano, thabiti, uwezo wa kuona na kufanya mambo yaliyo muhimu.

Baba mtakatifu mzaliwa wa Argentina mwenye umri wa miaka 79 pia alitumia hotuba yake kushinikiza baadhi ya ujumbe muhimu wa upapa wake kama huruma, uelewa na haki.

Amesema katika dunia ambayo mara nyingi haina huruma kwa mtenda dhambi na inakuwa na upole kwa dhambi, tunahitaji kuwa na tabia yenye dhana nzito kwa haki, kupambanua na kufanya anachotaka mwenyenzi mungu.

XS
SM
MD
LG