Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:29

Mahiga: Tanzania itatanzua mzozo wa Zanzibar bila ya msaada wa nje


Wafuasi wa CUF wakifurahia uwezekano wa ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 25
Wafuasi wa CUF wakifurahia uwezekano wa ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 25

Serikali ya Tanzania imeitaka umuia ya kimataifa kutoingilia kati suala la mzozo wa kisiasa la Zanzibar, ikieleza kwamba serikali ya mungano ya Tanzania inalishughlikia suala hilo na litapatiwa ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo.

Balozi Augustine Mahiga
Balozi Augustine Mahiga

Msimamo huo ulitolewa siku ya Jumanne na waziri wa manbo ya nchi za nje na ushirikiano wa Tanzania Dk Augustine Mahiga akizungumza kwa mara ya kwanza na mabalozi wa nchi za nje mjini Dar es Salaam.

Mahiga azungumzia Zanzibar na Burundi
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:40 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Balozi Mahiga, amesema kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi visiwani Zanzibar kunatokana na kuwepo kwa utamaduni tofauti wa kisiasa baina ya Bara na Zanzibar.

“Kwa hivyo demokrasia tunayozungumza, sisi hapa tunaiishi hiyo demokrasia. Na ninasema tizameni katika nchi za bara la Afrika, niambieni mahala ambapo uchaguzi hauna na matatizo. Lakini sisi tunaachiana madaraka na kwa Amani, bila utata.

Akizungumzia mgogoro wa Burundi waziri Mahiga amesema, Tanzania kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, imeamua kulishughulikia suala hilo kwa kufufua mchakato wa mazungumzo ya kisiasa yanayotarajia kuanza Desemba 28 na baadaye Januari 8.

Anasema pande zote zimekubali kushiriki kikamilifu.

Kuhusiana na kupelekwa kwa kikosi cha kulinda Amani la Umoja wa Afrika huko Burundi, Balozi Mahiga anasema Tanzania imeitaka Umoja wa Afrika kuvuta subira juu ya azma yake ya kupeleka wanajeshi wake elfu 5, na kutaka juhudi za mazungumzo ya kisiasa zipewe kipaumbele kabla ya kupeleka askari nchini Burundi.

XS
SM
MD
LG