Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:56

Rais Kabila Afanya Ziara Mji wa Vita


Rais Joseph Kabila wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amefanya ziara ya kutembelea mji wa Oicha, uliopo Beni, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa muandishi wa habari Austere Malivika aliyeshuhudia ziara ya Rais Kabila amesema kiongozi huyo ameahidi kupatikana kwa amani katika eneo hilo kwa haraka.

Ziara ya Rais Kabila ya Oicha imekuja wakati eneo hilo likiwa linakumbwa na mapigano yanayofanywa na vikundi vya uasi nchini DRC.

Vikundi ambavyo vinadaiwa kuvuruga amani ya eneo hilo inasemekana vinatoka nchini Uganda pamoja na raia wa nchi nyingine.

Unaweza kusikiliza taarifa ya mwandishi wetu Austere Malivika wa DRC.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:48 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


XS
SM
MD
LG