Umoja wa Afrika umesema hapo Alhamisi kwamba haupo tayari kuona yanatokea mauaji ya halaiki nchini Burundi.
Wakati umoja huo ukitoa tamko hilo, Umoja wa Mataifa imetoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi wa vitendo vilivyosambaa vya unyanyasaji na kuonya kutokea kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limesema kupitia ujumbe wa Twitter wakati wanachama wakijadili hali ya Burundi.
Baraza hilo limedai kwamba Afrika haitoruhusu kutokea kwa mauaji mengine ya halaiki katika ardhi yake.
Mauaji yanayoendelea yamesababisha dunia kutaka kumalizwa kwa ghasia nchini Burundi ambapo watu zaidi ya 400 wameshakufa toka mwezi Aprili.
Hoja za uchochezi zimekuwa zikizidi na kuzusha hofu kwamba nchi hiyo inaweza ikakabiliwa na tukio kama lililotokea nchini Rwanda